December 5, 2018


Kutokana na ushindi mnono walioupata klabu ya Simba jana wa mabao 4-0 dhidi ya Mbabane Swallows kwenye ligi ya mabingwa Afrika ugenini, inawezekana kauli ya Rais John Pombe Magufuli imekuwa kichocheo.

Simba imepata ushindi huo ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu Rais Magufuli awatake Simba wapambane ili kuweza kuchukua ubingwa wa Afrika kwani hakuna timu yoyote kutoka Tanzania ilishawahi kufanya hivyo.

Ikumbukwe katika mechi ya mwisho ya msimu wa ligi uliopita ambayo Simba walichapwa bao 1-0 na Kagera Sugar, Magufuli aliwataka Simba kupambana zaidi ili wafanikiwe kutwaa taji la Afrika.

Kauli hiyo inakuwa kama nguvu waliyopewa Simba na Rais Magufuli inayowafanya wapambane kwa namna wawezavyo ili kuhakikisha wanafanya vema kwa mashindano haya makubwa na ikiwezekana kuchukua kombe.

Ushindi wa mabao 8-1 unaonesha dhahiri shahiri kuwa Rais alitamka kitu ambacho kinapaswa kitekelezwe ili historia iweze kuwekwa hapa nchini kupitia Simba.

Baada ya mchezo wa jana, Simba sasa itakutana na Nkana Red Devils ama UD Songo ambazo zitakutana leo dimbani.

1 COMMENTS:

  1. Kama watanzania tumeamua kubadilika kuelekea katika ubora basi wakati ndio huu amabapo tueipata fursa yakuwa na kiongozi ambae anapigania na kusaidia na kuongoza kuelekea kwenye mabailiko ya kutuondoa katika unyonge kwani tusipokuwa tayari kubadilika sisi wenyewe chini ya kiongozi anaetutakia mema tutakuja kubadilshwa na watu au kiongozi anaetutakia mabaya. Kweli chungu lakini Tanzania na watanzania wanaanza kutengeza vichwa vya habari Duniani.Hii yote sio kwa bahati mbaya bali watanzania tulizoea ubabaishaji katika maisha na kazi zetu lakini makazo wa muheshimiwa Magufuli na serikali yake yakuwataka watanzania kuwa waadulifu na wa kweli katika kazi zao zianaanza kuzaa matunda kwa kasi ya ajabu. Tunaipongeza timu ya Simba na uongozi wake kwa kuchukua jitihada ya kufuata maelekezo ya muheshimiwa raisi katika kujenga taswira mpya ya Tanzania ya ushindani. Sisi Watanzania sio wanyonge bali tunajitakia unyonge wa makusudi.Na kwa bahati mbaya bado kuna wapumbavu wanaendesha kampeni kwa kupitia kisingizio cha uhuru wa siasa na haki za binaadamu kuwadumaza akili watanzania. Mfano mdogo tu mpe choice au uchaguzi mtanzania wa kuchagua wapi anataka kuishi kati ya Tanzania na Saudi Arabia? Hapana shaka katika watanzania kumi watajibu wanataka kuishi Saudi Arabia licha yakwamba hata unywaji wa kahawa unaweza kukutia matatizoni kwa kutumia kilevi. Umasikini ni kifungo kibaya kwa mwanadamu na uvunjifu wa haki za mwadamu namana moja lakini jiulize kuwa wazungu wanajali na kusikitishwa na hali duni za waafrica? Hakika hawajali hata kidogo zaidi ya unafiki.Na ili kujikomboa kutokana na umakini na unyonge kunahitaji nidhamu ya maisha inaoambatana na kufanya kazi kwa bidii chini ya uongozi unaojali na kuthamini juhudi za watu wake katika kujiletea maendeleo kwa bahati watanzania tumeipata serikali inayojali watu wake kilichobaki ni kufuata maelekezo hakika muda si marefu watanzania tutaondokana kuwa punching bag au kiroba cha kujifundishia kupiga kwa kuwa kila anaejifundishia kupiga iwe kimaisha,kimichezo,kiuchumi,kikazi akipangiwa na mtanzania anajua anakuja kupiga tu nakuondoka akituacha tukiteseka na machungu. Tanzania na watanzania kuna vipaji iwe kwenye elimu,michezo na kazi mbali mbali lakini ni wavivu wa akili na kimwili uiosindikwa na moyo wa kutamani kupata mafanikio bila ya kuyafanyia kazi au njia za kimagumashi na ndio maana watanzania tumechelewa kutoka. Walimwengu wanasema..the hard work beats the talent,when talent is doing nothing.Yale maneno yakwamba uchumi tunao lakini tungali masikini na wale wasiokuwa na uchumi au rasilimali za kutosha wana maisha mazuri kuliko sisi. Ndipo pale watu wanaposema jitihada katika kazi inafunika mwenye kipaji aliebweteka. Watanzania tunaweza tukiamua tena sana na kuishangaza Dunia ila tusitegemee mtu au nchi kuja kutuboreshea maisha yetu kamwe hatotokea tumeshasubiri sana na hakuna aliekuja kututoa shimoni.Mungu na huruma zake amemleta kiongozi wa kututoa hapa tulipo, watanzania lazima tushikamane nae ingawa kuna baadhi ya watanzania watakwazika ni kawaida kwani hata Nabii Musa aliua kabla ya kufanikiwa kuwaondoa wana wa Israeli chini ya udhalimu wa Ferauni na sina maana yakwamba raisi wetu auwe lahasha lakini kihistoria hakuna taifa lilonyanyuka kiuchumi na maendeleo ya kweli bila ya kupita kunako ubatizo wa moto.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic