December 5, 2018


Baada ya kuisambaratisha vibaya Mbabane Swallows nchini kwao kwa maba0 4-0 katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baadhi ya mashabiki wa Yanga wamewapongeza wachezaji wa Simba kwa nguvu waliyoitumia kuhakikisha wanapata matokeo.

Mashabiki hao wameamua kufunguka kwa kutoa pongezi zao kwa wachezaji wa Simba kutokana na kuiwakilisha nchi kwenye mashindano makubwa ambayo msimu uliopita Yanga walishiriki.

Baadhi yao wameeleza kuwa kwa namna kikosi cha timu hiyo kilivyo walikuwa wanaamini watapata matokeo na imetokea kama ambavyo walikuwa wanategemea.

Hawakusita kuwatakia kheri katika hatua nyingine inayofuata ili waendelee kuitangaza Tanzania vizuri na ikiwezekana waweze kuchukua ubingwa wa Afrika ili kuleta heshima kubwa ndani ya soka la Tanzania.

Kutokana na ushindi wa mechi ya jana, Simba imefanikiwa kuwabugiza mabao 8-1 Mbabane ikiwa ni baada ya mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezewa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 4-1. 

2 COMMENTS:

  1. Nayale mabango ya uzendo mwisho ..... Yalitoka wap au walizan nitim ya 250 yanga bhana mnakela

    ReplyDelete
  2. Jamaa wanapata TABU SAAAAANA! Ila kwa wale wachache wanaoijua radha ya mpira, ni lazima watasifu kiwango cha Simba hata kama damu yako ni ya kijani. Yaani Simba hii INAKATA NYUMBANI halafu INAFUNULIA UGENINI (Hii ni kata funua).

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic