MAKAMBO AMPIGA MKWARA MZITO KAGERE
Licha ya kushindwa kufunga jana dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya, mshambuliaji wa timu hiyo, Mkongoman, Heritier Makambo, ni kama ameanza nyodo vile baada ya kuwafikia washambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kwenye idadi ya mabao ya kufunga.
Makambo, Alhamisi ya wiki jana alifikisha mabao saba ambayo yamefungwa na Okwi na Kagere wakati Yanga ilipocheza na Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Taifa na matokeo. Yanga ilishinda 3-0.
Mkongoman huyo aliyefunga mabao matatu kwenye mechi tatu mfululizo za ligi za hivi karibuni, anamfukuzia mshambuliaji wa Mbeya City, Eliud Ambokile, anayeongoza katika ufungaji akiwa amaepachika mabao nane. Tofauti ni bao moja tu.
Makambo alisema moja ya malengo yake aliyoyapanga ni kuona anaendelea na kasi yake ya kufunga mabao katika michezo inayofuata ya ligi.
Makambo alisema, kasi yake ya kufunga mabao imerejea baada ya kuyafanyia kazi makosa yaliyokuwa yanamsababisha ashindwe kupachika mabao huku akifuata maelekezo ya kocha wake, Mwinyi Zahera kabla na baada ya mechi.
“Nimejifunza vitu vingi kwa kipindi kifupi nilichokuwa Yanga, kwa kifupi mashabiki wanapenda kuona timu yao ikipata matokeo mazuri ambayo siyo ya kufungwa, wao wanapenda ushindi tu.
“Katika mechi za hivi karibuni kabla ya kwenda Shinyanga kucheza Mwadui FC, mashabiki walikuwa wanabeza kiwango changu kwa kuanza kuniongelea vibaya, lakini nashukuru maneno hayo haya kunitoa mchezoni zaidi nili ongeza bidii ya mazoezi na kuongez a umakini katika kufunga mabao.
“Nikaanza kufunga mechi na Mwadui na michezo mingine iliyofuat a nikaendelea kufunga ikiwemo na Kagera Sugar kabla ya kucheza na JKT Tanzania ambayo nayo nilifunga, hivyo nimepanga kuendelea na kasi yangu hii ya kufunga mabao,” alisema Makambo.
0 COMMENTS:
Post a Comment