December 4, 2018


Na George Mganga

Ofisa Habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, amewataka waamuzi wa mechi za Ligi Kuu Bara kuhakikisha wanachezesha mechi kwa kufuata sheria 17 za mchezo wa soka.

Kauli hiyo imekuja mara baada ya mechi ya Tanzania Prisons dhidi ya Yanga kumalizika kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Yanga kushinda kwa mabao 3-1.

Ten amesema kuwa inawezekana kuna mpango wa kuvuruga mechi za Yanga ili kuiharibia kupata matokeo jambo ambalo si rafiki kwa mchezo wa soka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ten ameandika kwa uchache juu ya madhaifu akilenga waamuzi waliochezesha mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic