BAADA ya kikosi cha Ruvu Shooting kupapaswa na Lipuli FC katika mchezo wa Ligi kuu kwa kuchapwa bao 2-1, Ofisa habari Masau Bwire ameamua kukimbilia kwenye milima ya Odzungwa mkoani Morogoro ili kupunguza maumivu.
Bwire ameungana na msafara wa walimu wa shule za Msingi Manispaa ya Kinondoni kufanya ziara ya utalii wa ndani kwa kuzuru maeneo kadhaa ya kitalii ndani ya nchi.
"Tumesafiri hadi Mang'ula, Ifakara, mkoani Morogoro ambapo tulilala ili asubuhi hii tupande mlima Odzungwa, baadaye tuzuru mgodi wa kuzalisha umeme kidatu na bwawa la kidatu, baada ya hapo tutasafiri hadi Iringa ambapo kesho tutatembelea mbuga ya kuhifadhi wanyama ya Ruaha, kisha Kalenga kulikohifadhiwa fuvu la chifu Mkwawa.
"Ni vizuri na inapendeza kufanya utalii wa ndani kwa gharama nafuu sana ili kuyajua na kujifunza mambo mbalimbali yaliyoo katika maeneo ya kitalii na vivutio vyake ndani ya nchi yetu, pia kupunguza stress kama sio kuondoa kabisa stress zinazotuhangaisha," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment