December 12, 2018


Kocha Mkuu wa Mbao FC, Amri Said amesema kuwa kinachoiponza timu yake kushindwa kupata matokeo kwenye ligi ni uchovu pamoja na kutokuwa na kiungo katika kikosi chake.

Mbao jana walikubali sare ya kutofungana dhidi ya African Lyon na mchezo wake uliopita dhidi ya Azam FC alikubali kichapo cha mabao 4-0.

"Mapungufu makubwa ambayo yapo kwenye kikosi changu ni kutokana na uchovu wa kikosi changu, ila matokeo kwenye mpira ni ya kushangaza, tutaendelea kupambana ili kuweza kupata matokeo katika michezo yetu inayofuata," alisema.

Mbao wamecheza michezo 15 kwenye ligi wakiwa nafasi ya 9 baada ya kujikusanyia jumla ya pointi 20.

1 COMMENTS:

  1. Mbao wakeshaikamia Simba basi kazi imekwisha. Wanadhani ligi nzima ni kuifunga Simba basi. Kutumia nguvu zote kwa kutaka kujionesha kwenye mechi moja ni ujinga wanatakiwa kupambana mwanzo mwisho sio mechi moja halafu inabakia kuwa kibonde kwa timu nyengine TOTO Africa ilipotea kwa staili hiihii ya Mbao.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic