December 5, 2018


Na George Mganga

Mwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' amefurahia ushindi wa timu yake ilioupata jana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuisambaratisha Mbabane Swallows mabao 4-0 ikiwa kwao Swaziland.

Simba ilifanikiwa kuibuka na mabao hayo na kufanikiwa kuingia hatua ya kwanza ya mashindano ambapo sasa itacheza na kati ya mshindi baina ya Nkana Red Devils ya Zambia na UD Songo ya Msambiji zitazovaana leo huko Zambia.

Kutokana na matokeo hayo, Mo amewapongeza Simba na kuwataka wajipange vilivyo ili kujiandaa na hatua ijayo kwa mechi itakayofuata waweze kuendelea ushindi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mo ameandika akieleza kuipongeza timu na kuiasa ijipange vema kuelekea mchezo utakaofuata.







2 COMMENTS:

  1. Hongera sana Mo kwa upendo wako na sapota ya hali ya juu kufanikisha matokeo haya matamu kwa Simba na kwa watanzania, na Mungu amubariki sana. Watanzania na wanasimba wanathamini sana mchango wako na wanakupenda sana kwani ulipopatwa na mtihani nchi yote ilinyong'onyea ni furaha kusherekea ushindi huu mnono tukiwa pamoja Aamin.

    ReplyDelete
  2. Hongera Simba (Wanachama, Mashabiki, Benchi la ufundi, Uongozi wa Timu, Uongozi wa Club, Safu ya mwekezaji Mkuu). Ndio maana naipenda Simba. Kama huipendi Simba kaa kimya!. Acha cc tule raha na Simba yetu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic