December 4, 2018


Imeelezwa kuwa uongozi wa Mbabane Swallows ya Swaziland umetishia kuishitaki klabu ya Ya Simba katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kutokana kuonesha vitendo vinavyoashiria ni vya ushirikina.

Taarifa imeeleza kuwa, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Novemba 28 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, uongozi wa Mbabane umedai kuwa kiongozi mmoja wa Simba walimuona akinyunyuzia maji katika njia inayoelekea upande wa vyumba vya kubadilishia nguo vya wachezaji wa Mbabane.

Kutokana na kitendo hicho, Mbabane wanaamini kuwa inawezekana ikawa sababu ya kufungwa mabao manne na Simba kwenye mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa Mbabane kufungwa mabao 4-1.

Wakati Mbabane wakitangaza kuwastahki Simba CAF, timu hizo mbili zitashuka dimbani kucheza mechi ya marudiano leo itakayoanza majira ya saa 10 na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba inatakiwa kwenda suluhu pekee kwenye mechi hiyo ili kujitengenezea nafasi nzuri ya kusonga mbele mpaka hatua inayofuata.

5 COMMENTS:

  1. Acheni upuuzi uchawi hauchezi mpira,acheni nizamu ya uoga mbona mapema sana alafu kama kushinda Mbabane mna nafasi kubwa sana,hizi timu za Tanzania hazina kitu mnaweza muwapige hata sita hao wanaojiita simba,hayo maengine haryana nafasi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Timu ya kufungwa sita ni yanga sio simba acha kuwadanganya

      Delete
  2. Mbona hata wao walimwaga maji kabla ya kushuka kwenye gari walikuwa na maana gani wameshaingiza upepo hao wanatafuta pakutokea

    ReplyDelete
  3. Sababu za kufeli mtihani huwa nyingi sana! Jamaa wameanza sababu. Sasa kama Simba waliwafunga kwa ushirikina, leo si wapo kwao, iwapo wao wana uwezo mkubwa kuwazidi Simba, basi wawafunge huko kwao. Ila wakishindwa kuwafunga, basi wao ndo watakuwa wadhaifu kupitiliza. @ KEYA SAID - Tangu niifahamu Simba, Sijawahi kusikia wala kuona ikipigwa goli tano au sita kimataifa, mzee tafuta rekodi. Ila naungana nawe kuwa UCHAWI HAUCHEZI MPIRA, hizo ni dalili za uoga tu na kuifanya Simba ionekane ni timu dhaifu kwao.

    ReplyDelete
  4. Mbinu za kimpira hizo wameshapigwa hao

    Pro

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic