Wawili hao wametumia muda mwingi kucheza nafasi ya ukabaji, lakini fei Toto ameweza kufunga mabao 2 katika michezo 14 ambayo amecheza huku mkude katika mechi 12 alizocheza hajafunga hata bao moja.
Mabao aliyofunga Fei Toto ni katika mchezo wao dhidi ya KMC ambapo alifunga bao la usiku na lile dhidi ya Ruvu Shooting ambalo alifunga akiwa nje ya 18.
Mchambuzi wa masuala ya mpira, Mwalimu Kashasha amesema kuwa inatokana na namna ya maelekezo ya mwalimu kwa wachezaji wake wakiwa uwanjani anataka wafanye nini na wakati gani ila wote ni wachezaji makini na wanajuhudi uwanjani.








0 COMMENTS:
Post a Comment