December 23, 2018


Hii ni kali. Unaambiwa shabiki mmoja kindakindaki wa Simba ameamua kuahirisha safari ya kwenda Moshi kwa ajili ya kuitazama timu yake leo ikimenyana na Nkana Red Devils ya Zambia kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mchezo wa mkondo wa pili ikiwa na kumbukumbu ya kulazwa mabao 2-1 huko ugenini Zambia.

Kwa mujibu wa Radio One, shabiki huyo ametamba kuwa Simba itafanya vizuri na kuwashangaza wengi akiamini kikosi kipo vizuri na haoni wapi Nkana watatokea leo.

Ameeleza kuwa safari ya Moshi ameona haina umuhimu hivi sasa na akitaka kuishuhudia Simba ikifanya maajabu ikiwa ni timu pekee iliyosalia kwenye mashindano ya kimataifa baada ya Mtibwa kuondolewa jana na KCCA.

Shabiki huyo ametamba kwa kujieleza kuwa yeye ni mchaga ORIJINO na baada ya mechi ataondoka na gari lake binafsi kesho yake tayari kwa kwenda kula sikukuu ya Krismani ambayo itakuwa Disemba 25 2018.

1 COMMENTS:

  1. Iwe sikukuu ya Christmas na na ushindi wa mnyama. Tumuombe Mungu mnyama angurume leo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic