December 23, 2018


Wakati wapenzi na wadau wa soka nchini Tanzania wakisubiria kwa hamu mtanange wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba dhidi ya Nkana, baadhi ya mashabiki wa Yanga wametoa tathimini ya mchezo huo.

Mashabiki hao walio na moyo wa uzalendo wametaka Simba kupigana kwa nguvu zote kuhakikisha timu yao inafanya vema ili kuitangaza nchi vizuri.

Baadhi wamesema hawapaswi kucheza mchezo wa kujilinda sana pale watakapopata bao la kuongoza kwakuwa watakuwa wanakaribisha hatari langoni mwao.

Aidha, wameushauri uongozi kuwapa somo la saikolojia wachezaji wao ili kuhakikisha wanaingia uwanjani wakiwa na akili ya kusaka matokeo mazuri pekee na si kupoteza imani ya ushindi.

Simba inapaswa kupata ushindi wa bao 1-0 na isiruhusu wave wake kuguswa ili kujiwekea nafasi nzuri ya kusonga mbele kuelekea hatua nyingine ya mashindano.

3 COMMENTS:

  1. Tathimin Nzuri Sana Na Niwachache Lakin Bado Nao Ni Wanafiki Tukipoteza Watafurahi! Kwamba Simba Tukifunga Yanga Watafurahi? Hawawezi Kabisa

    ReplyDelete
  2. Baada ya vipers ya Uganda na Gormahia ya kenya kushindwa kuingia hatua ya makundi matumaini pekee Africa mashariki yamebaki kwa Simba. Kwa hivyo watanzania na wana Africa mashariki hawana budi kuinga mkono Simba kwa nguvu zote kesho.

    ReplyDelete
  3. Ushindi wa timu za nyumbani ni ushindi na heshima kwa nchi yetu ikiwa simba, yanga, azam au timu yeyote nyengine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic