December 15, 2018


Bosi mmoja wa juu ndani ya Klabu ya Simba, ameshawasili nchini Afrika Kusini na kukutana na mabosi wa Kaizer Chief kwa ajili ya kukamilisha dili la Emmanuel Okwi raia wa Uganda.

Okwi ambaye mkataba wake na Simba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, anatakiwa na Kaizer Chief ambapo timu hiyo imeweka mezani mzigo wa maana ambao Simba wamekubali kuuchukua na kumuachia nyota wao huyo.

Hivi karibuni Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ aliripotiwa kuridhia usajili huo wa Okwi ambapo alikutana naye na kuzungumzia ishu hiyo ya kwenda Sauz.

Chanzo kutoka ndani ya Simba kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, hivi karibuni, bosi huyo ambaye hakupenda kumtaja jina lake, alifika Afrika Kusini kwenye makao makuu ya Kaizer Chief kwa ajili ya kumalizana kwenye dili hilo.

Mtoa taarifa huyo aliongeza kuwa, Kaizer Chief wameweka mzigo wa maana ambao Simba wamekubali kuuchukua kwani wanaona wakizembea wanaweza kumuona Okwi akiondoka bure mwishoni mwa msimu huu.

“Ni kweli kuna kiongozi wa juu kabisa wa Simba amefika Afrika Kusini na kukutana na mabosi wa Kaizer Chief kujadiliana dili hilo la Okwi.

“Kila kitu kimekwenda sawa na muda wowote tunaweza kuona Okwi anaondoka Simba na kwenda kuyaanza maisha mapya huko Afrika Kusini.

“Wale jamaa wamemuandalia Okwi mshahara ambao unazidi Sh milioni 30, lakini pia Simba ikimuuza itaambulia kitita si chini ya Sh milioni 300.

“Kutokana na fedha hizo za usajili kuwa nyingi, hakuna ambaye amekataa kwa sababu Okwi mwenyewe mkataba wake umebaki takribani miezi saba, sasa kama wakimzuia anaweza kuondoka bure mwishoni mwa msimu,” kilisema chanzo.

5 COMMENTS:

  1. Dah Ila Okwi Kutoka Simba Basi Japo Tuna Chama Lakini Mtu Kama Okwi Simba Alikuwa Ni Wa Mhimu

    ReplyDelete
    Replies
    1. amekuwa akiondoka na kurudi bado Simba ipo. Kwa hiyo sio dhambi wala Simba haitateteleka

      Delete
  2. Salamba atapata kuchukuwa pahala pake adhihirishe makali yake na tunamtakia Okwi kila la heri

    ReplyDelete
  3. Alitakiwa aende yeye au kaizer waje hapa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic