MRITHI WA MOURINHO MAN UNITED HUYU HAPA
Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kurithi mikoba ya Jose Mourinho ambaye amefutwa kazi na Manchester United, ila itawalazimu United kuilipa Spurs dau la pauni milioni 34 kama watataka kumpeleka mkufunzi huyo raia wa Argentina katika uga wa Old Trafford . (Times)
Kocha wa Real Madrid Santiago Solari amesema hana wasiwasi wowote juu ya tetesi kuwa Mourinho anatarajiwa kuchukua kazi yake. (Sky Sports)
Mourinho amekaa siku 895 katika hoteli ya The Lowry wakati akiifundisha United, na gharama za kuishi hapo zimefikia pauni 537,000. (Guardian)
Zaidi ya asilimia 90 ya wachezaji wa Manchester United walikuwa hawamtaki Mourinho - na hata wale wachache ambao walikuwa wakimpenda walihisi muda wake wa kuondoka klabuni hapo umetimia. (Independent)
Msaidizi wa muda mrefu wa kocha wa zamani na gwiji Sir Alex Ferguson, bw Mike Phelan anatarajiwa kurudi Old Trafford akisaidiana na kocha wa muda Ole Gunnar Solskjaer mpaka mwisho wa msimu. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro Morata, 26, anatarajiwa "kurudi Italia hivi karibuni", huku taarifa zikionesha kuwa anaweza kujiunga na miamba AC Milan. (The Sun)
Harakati za Arsenal kumsaini mchezaji wa Real Madrid Isco, 26, zinaoneka kugonga mwamba baada ya kudaiwa kuwa Manchester City tayari wameshaanza mazungumzo na nyota huyo wa timu ya taifa ya Uhispania. (The Sun)
Klabu ya Crystal Palace ipo mbioni kumsajili kwa mkopo mchezaji wa Liverpool Dominic Solanke, 21, kwenye dirisha la usajili la mwezi ujao, Januari. (Evening Standard)
Atletico Madrid hawatazamiwi kuongeza mkataba wa beki wao wa kushoto Filipe Luis, 33. (Marca)
Paris St-Germain hawatamuachia Adrien Rabiot anayewindwa na Liverpool kuondoka kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu baada ya kukataa kuongeza mkataba wake. Klabu hiyo inapanga kumpiga bei kiungo huyo mwenye miaka 23 pale dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi ujao. (L'Equipe)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment