December 19, 2018


Licha ya hivi karibuni mwanamuziki wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini ‘Dudu Baya’ au Konki Konki Konki Master’ (pichani) kunaswa akiwa amelainika kwa msanii, Gift Stanford ‘Gigy Money’, wikiendi iliyopita alimshushia mwanadada huyo kipigo cha aina yake. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita jijini Mwanza ambapo inaelezwa ugomvi ulianza kama utani wawili hao wakiwa nyuma ya jukwaa wakati Tamasha la Wasafi Festival likiendelea.

Shuhuda wa tukio hilo alidai Gigy ambaye mara nyingi ameonekana akiwa karibu na Dudu Baya alikuwa akiongea sana na kutaja mambo ambayo ni matusi mbele za watu huku Dudu Baya naye akiwa na mwanaye.Wakati Gigy akiendelea kumwaga maneno ya chumbani akijihusisha na Dudu Baya, msanii huyo mwenye asili ya utata alikuwa kimya kwa aibu akiwa na binti yake, Maria.

Kukaa kimya kwa Dudu Baya hakukusaidia kitu kwani Gigy aliendelea kutoa maneno makali lakini yalipozidi mwanamuziki huyo aliwaomba waungwana wakamtulize mwanamama huyo. “Yaani maneno ya Gigy yalikuwa yanamfadhaisha sana Dudu Baya na mwanaye  ambapo licha ya kumtaka aache hakusikia, aliendelea tu,” alidai shuhuda.

Kutokana na kuendelea kutoa maneno machafu Dudu Baya alimvaa Gigy na kumshushia kipigo cha ambapo aliokolewa na mabaunsa waliokuwa karibu. Katika varangati hilo Gigy aliangua kilio kutokana na maumivu huku akilalama kupoteza simu yake ya kisasa. Baada ya kutokea kwa sakata hilo, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na Dudu Baya ili kueleza sababu za kumshushia kipigo Gigy na kufunguka;

“Huyu Gigy hana akili, nilishamwambia muda mrefu kwamba sitaki utani wake yeye hanielewi, yule ni mwanamke wa ajabu sana.” Kwa upande wa Gigy alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo aliomba aachwe aitafute simu yake. “Hebu niache bwana, nimeshapoteza simu yangu na wewe unanichanganya tu,” alisema Gigy.

Kutoka Global Publishers

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic