December 26, 2018


KIKOSI cha Mtibwa Sugar kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kiluvya United ambayo kwa sasa inaitwa Rufiji United katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliochezwa uwanja wa Manungu, Mkoani Morogoro.

Ofisa habari wa Rufiji United, Steven Kinabo alitabiri ushindi wa mabao 3 kwao hali iliyofanya matokeo kubadilika na wao kufungwa bao hizo ugenini na kutolewa nje kwenye mashindano ya Shirikisho.

Mabao ya Mtibwa Sugar leo yalifungwa na Kelvin Sabato aliyezifumania nyavu mara mbili dakika ya 6 na 38 na bao la mwisho likipachikwa na  Haruna Chanongo dakika ya 46.

Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa Sugar kusonga mbele katika hatua ya 4 wakiwa na nafasi ya kuweza kulitetea taji lao tena msimu huu kwa kuwa bado lipo mikononi mwao.

4 COMMENTS:

  1. Matokeo ya mabingwa wa nchi na wakigoma mbona mnayaficha?

    ReplyDelete
  2. Hakuna Kilicho Fichwa Simba 2 - 3 Mashujaa

    ReplyDelete
  3. Maskini wenye kikosi kipana cha kimataifa

    ReplyDelete
  4. Kosa si Kosa ila kosa ni kurudia kosa....mwaka jana tuliidharau Green Warriors wakatutoa mwaka huu mashujaa hizi timu hata hazifahamiki....Hapa kuna shida moja kubwa ya dharau, kutojituma na kuridhika hii ni hatari ikiendekezwa itaigharimu Simba.....hawa wachezaji wanatimiziwa mahitaji yote lakini hakuna fighting spirit

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic