December 26, 2018





Mshambuliaji nyota wa Yanga, Heritier Makambo na beki wa timu hiyo, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, wamekabidhiwa viatu vipya vya kuchezea kutoka nchini Uturuki.


Nyota hao wamekabidhiwa viatu hivyo jana Jumatano na Mzee Karama ambaye ni mdau mkubwa wa soka hapa Tanzania. Mbali na viatu, pia Makambo alikabidhiwa mpira.


Mdau huyo mwenye duka la vifaa vya michezo la Just Fit lililopo Mlimani City jijini Dar, aliwakabidhi viatu hivyo dukani hapo na wenyewe wakiahidi kuanza kuvitumia katika mchezo wao ujao dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Baada ya kuwakabidhi, Mzee Karama alisema: “Kutokana na Makambo kunifurahisha kwa namna ya anavyofunga mabao, nimeona nimzawadie hivi viatu na huu mpira ili aendelee kujifua zaidi na aendelea kufunga.

“Kwa upande wa Ninja, nimempa viatu kwa sababu nimeona anajituma katika nafasi yake ya ulinzi, lakini pia ndiye beki mwenye mabao mengi kwa sasa, naamini zawadi hii itamfanya awe bora zaidi.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic