Mshambuliaji wa timu ya Simba Emmanuel Okwi, raia wa Uganda amepewa kazi maalumu ya kuivusha Simba kwenye hatua ya makundi kwa kushirikiana na wachezaji wenzake ili kuwafunga mabao zaidi ya 2 Nkana FC ya Zambia.
Simba wanawakilisha Taifa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ili waweze kufika hatua ya makundi wanapaswa wawafunge Nkana bao 1-0 katika mchezo wa marudio utakaochezwa Jumapili kwa kuwa mchezo wa kwanza walikubali kupigwa bao 2-1 ugenini.
Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelu, 'Julio' amesema safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Okwi inapaswa ifanye jitihada ya kufunga mabao zaidi ya 2 ili kuvuka hatua ya kwanza.
"Simba ni timu kubwa na ina wachezaji makini, sasa ili wafanikiwe kuvuka hatua ya kwanza wanapaswa wafunge zaidi ya mabao 2 wasibweteke na bao 1 la ugenini mpira unadunda nao wanapaswa watumie akili uwanjani kutafuta matokeo katika uwanja wa nyumbani.
"Okwi, Kagere na wachezaji wote wa Simba wanapaswa waelekeze akili zao katika mchezo wao wa kimataifa wanauwezo wa kuvuka hatua hii endapo watajitambua na kupambana kwa hali na mali," alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment