December 3, 2018





Wachezaji wa Simba wameuahidi uongozi wa klabu hiyo kwamba watapambana na kuvuka dhidi ya Mbabane Swallows ya eSwatini.

Tayari Simba iko eSwatini na Mtendaji Mkuu wa Simba, Clescentius Magori amesema wachezaji wamewaahidi kufanya vema.

"Wachezaji wa Simba wanajitambua, wanajua umuhimu wa michuano hii na wameahidi kupambana vilivyo kuhakikisha wanashinda mchezo huu," alisema Magori ambaye ameongozana na timu hiyo nchini eSwatini.

Magori ameelezea kuhusiana na maandalizi na kusema kila kitu kinaendelea katika mpangilio ulio bora kabisa na wao wamejiandaa vilivyo.

Katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo jijini Dar es Salaam, Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Taifa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic