December 3, 2018




Huku wapenzi  na mashabiki wa soka hapa nchini wakiendelea kujiuliza wapi Yanga inapata fedha za kuisafirisha timu hiyo kwa ndege kwenda mikoani katika mechi zake za Ligi Kuu Bara huku ikikabiliwa na ukata mkubwa, uongozi wa timu hiyo umeweka mambo hadharani.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samwel Lukumay amesema kuwa sababu kubwa ya kuisafirisha timu hiyo kwa ndege kwenda kucheza mechi zake za mikoani ni kuwaepusha wachezaji na uchovu wa barabarani ambao wangeupata kama wangetumia usafiri wa basi.

Alisema mbali na uchovu, pia kitendo cha kuwasafirisha kwa ndege ni kuwajenga kisaikolojia wachezaji wa timu hiyo kuhakikisha wanapambana vilivyo katika mechi zao hizo ili waweze kupata ushindi tofauti na ambavyo wangecheza kama wangesafiri kwa basi.

“Ni kweli kabisa hatuna fedha lakini tumekuwa tukipambana kuhakikisha timu yetu inafanya vizuri katika mechi zote ambazo inacheza nyumbani na ugenini.

“Hata hivyo, katika mechi za ugenini ambazo tunacheza mbali, kocha wetu mkuu alitushauri tuhakikishe tunawasafirisha wachezaji kwa ndege ili tuweze kufanya vizuri.

“Sababu kubwa ni kuwafanya wasichoke sana lakini pia hali hiyo itasaidia kuwajenga kisaikolojia japo kuwa kuna baadhi ya stahiki zao wanadai lakini wataona kuwa pamoja na kutudai bado tunawathamini, tofauti na ambavyo tungewasafirisha kwa basi zaidi ya masaa 12,” alisema Lukumay.

Mpaka sasa Yanga imewasafirisha kwa ndege wachezaji wake kwenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC na kisha Bukoba kucheza na Kagera Sugar na kisha wakarudi Dar es Salaam kwa kutumia usafiri huo na juzi Jumamosi wachezaji hao wamesafiri tena kwenda Mbeya kucheza na Prisons kwa ndege.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic