December 23, 2018


Unaweza kusema ni 'Mwendo Mdundo kwa Simba' baada ya leo kumefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Nkana FC ya Zambia katika mchezo wa marudiano uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanaipa nafasi Simba kutinga hatua ya Makundi baada ya kufanikiwa kushinda kwa jumla ya mabao 4-3 kwa kuwa mchezo wa kwanza walishinda kwa jumla ya mabao 2-1 na leo wapinzani wao wamekubali kupigwa mabao 3-1.

Nkana walikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Walter Bwalya na kuwafanya Simba waongeze kasi na kusawazisha dakika ya 26 kupitia kiungo Jonas Mkude aliyemalizia pasi ya Claytous Chama na dakika ya 45 Meddie Kagere alifunga bao la 2 kwa kichwa akimaliza pasi ya James Kotei.

Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kwa kumtoa Meddie Kagere dakika ya  56 nafasi yake ikachukuliwa na Hassan Dilunga na Emmanuel Okwi alitoka dakika ya 79 akaingia Shiza Kichuya hali iliyoweza kuongeza mashambulizi.

Iliwalazimu Simba wasubiri mpaka dakika ya 88 ambapo Hassan Dilunga alipiga pasi kwa guu la kushoto iliyomkuta Claytous Chama na kumalizia kwa kutumia kisigino kilichomchanganya mlinda mlango wa Nkana FC.

Matokeo hayo yanaipeleka Simba kwenye hatua ya Makundi kibabe huku kikosi cha Nkana FC kikishuka kupambana kwenye mashindano ya kombe la Shirikisho. 

1 COMMENTS:

  1. Wamesema sana na leo wameamua kumaiza kiu yao. Simba inakwenda kimataifa tena kwa mara nyingine.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic