December 12, 2018


Shirikisho la Soka Tanzania Bara limesisitiza kutoongeza siku za usajili wa wachezaji pindi dirisha dogo litakapofungwa rasmi.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Mario Ndimbo, amesema kuwa dirisha hilo litafungwa Disemba 15 ikiwa ni Jumamosi ya wiki hii kama ambavyo ilikuwa imepangwa na hakuna siku itakayoongezwa.

Ndimbo amesema mfumo unaotumika katika kufanya usajili ni uleule wa TFF FIFA Connnect na si vingine utaendelea na kazi mpaka tarehe ya mwisho ambayo ni 15.

Tayari baadhi ya timu zimeshasajili wachezaji kadhaa ikiwemo Simba na Azam FC huku Yanga ikitajwa kuwa kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji kwa ajili ya kumalizana nao.

Wakati huo timu zingine pia kama Singida United tayari imeshafanya maboresho ya kikosi chake kwa kusajili wachezaji kadhaa kutokana na timu hivi karibuni kuyumba kiuchumi suala lililosababisha baadhi ya wachezaji kuikimbia timu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic