Kocha msaidizi wa Mbao FC, Ally Bushiri ambaye ameajiriwa akitokea timu ya Njombe Mji, kukinoa kikosi cha Mbao, ameanza kwa kuangukia pua katika mchezo wake wa kwanza baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Dar City ya Tanga.
Mchezo huo uliopigwa jana katika uwanja wa CCM Kirumba ulikuwa ni wa kombe la Shirikisho ambapo dakika tisini zilimalizka kwa sare ya kufungana 1-1 na kufanya zipigwe penati ambapo Mbao walishinda penati 2 na Dar City wakashinda 4.
Mshambuliaji wa Mbao FC, Said Khamis amesema matokeo waliyopata yana maumivu ndani yake hivyo wanajipanga kwa ajili ya wakati mwingine kufanya vizuri.
"Tumeshindwa kupata matokeo wakati huu, hakuna haja ya kujutia sana kwa kuwa kila timu inastahili kushinda, kwa sasa muhimu kujipanga kwa ajili ya michezo yetu mingine," alisema.
Kocha Mku wa Mbao, Amri Said ameachana na Mbao kiroho safi baada ya kukubaliana na uongozi wa timu kwa kile alichoeleza kutoweza kufanya kazi na Bushiri ambaye wapo sawa kitaaluma kwenye elimu ya ukocha wote wakiwa na leseni B.
0 COMMENTS:
Post a Comment