Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kinachomsafikisha kwenda Ufaransa ni “kusinya” makaratasi na atarejea nchini Desemba 25.
Neno “kusinya” ana maanisha ni kusaini makaratasi, huku akisisitiza yanahusiana na biashara zake.
Maneno yake hayo yanafanya kauli ya safari yake iwe imegawanyika mara tatu kwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili alisema anakwenda Urafansa kwa ajili ya kesi inayomhusu yeye na mkewe.
Msemaji wa Yanga, Dismas Ten, yeye akasema kocha huyo anakwenda katika matibabu nchini Ufaransa na Zahera amesema anakwenda kusaini makaratasi yanayohusiana na biashara zake nchini Ufaransa.
Pamoja na mchanganyiko huo, Zahera ameweka msisitizo kwamba anakwenda nchini humo na atarejea Yanga.
“Wanaosema ninaondoka si kweli, mimi nawafundisha wachezaji wangu kuwa wavumilivu. Hivyo siwezi kukimbia matatizo,” alisema kocha huyo raia wa DR Congo.
0 COMMENTS:
Post a Comment