December 17, 2018





Suala la Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kuondoka nchini kwenda Ufaransa limezua mkanganyiko mkubwa hasa baada ya viongozi wa Yanga kujichanganya.


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika amesema kocha anakwenda Ufaransa kwa ajili ya kesi yake na mkewe.


“Ni kesi, tena hili suala lilikuwepo na atarudi baada ya kesi,” alisema.

Nyika amesema kesi hiyo imechukua miaka minne ndio na Zahera raia wa DR Congo anatakiwa kwenda kwa ajili ya hukumu.


Pamoja na Nyika kusema hivyo, Msemaji wa Yanga amesema kocha huyo anakwenda kwenye matibabu.


“Atachukua kama siku nne au wiki hivi kwa ajili ya matibabu na baada ya hapo atarejea na kuungana na timu,” alisema Dismas Ten.

Hali hiyo imezidi kuzua mkanganyiko huku asilimia kubwa ya mashabiki wakilaumu kuhusiana na hali hiyo.


6 COMMENTS:

  1. Hajalipwa huyo, simba timueni mzungu mchukueni zahera

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh huyo kocha wa nini msimbazi?anazungumza sana.mbona makocha kama Hans Plujim wako kimya na timu haijapoteza mechi hadi sasa.Tunasubiri bingwa ndio hukumu

      Delete
  2. Na bado watajichanganya sana.ameshamaliza mzunguko wake kwa makubaliano yao wanaojua hilo wametulia.

    ReplyDelete
  3. Mtu ana mambo yakebinafsi kwa nini yawekwe hadharani ni kosa kwa kweli. Kama ana matatizo na mkewe hakuna sababu ya kuwekwa hadharani hapa

    ReplyDelete
  4. Nyika katika viongozi makopo wa yanga ni huyu jamaa, yupo ki maslai sana yanga, hana faida kabsa yanga pale

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic