December 17, 2018






Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema ilibaki kidogo aondoke Yanga baada ya kudanganywa na viongozi wa usajili.

Zahera amesema alitaka kuondoka kwa kuwa alipendekeza wachezaji na akaahidiwa kuwa watafuatiliwa na kusajiliwa.

“Baada ya kuzungumza nao wakaniambia yule mshambuliaji wa Uganda tayari wamemamlizana naye, watakwenda  kumsainisha.

“Kama haitoshi walisema yule kipa Mkenya pia watakutana naye Kenya na kumalizana naye kama ilivyokuwa kwa mchezaji mwingine yule wa Mwadui.

“Saa nne usiku, wananipigia kwamba mchezaji wa Mwadui hatasaini. Vipi wakati walisema wamemalizana na wakanihakikishia kuwa kila kitu safi. Walimalizana naye vipi?”

“Hii ndio ilikuwa mipango yangu, imevurugwa na kweli kama sitachukua ubingwa, nisiulizwe. Waulizeni hao viongozi, hii si sawa, nimechukizwa sana,” alisema akionekana kuchukizwa na namna mambo yalivyokwenda.

Taarifa zinaeleza kamati ya usajili inayoongozwa na Hussein Nyika ilimuaminisha Zahera kila kitu kilikuwa safi ingawa mambo hayakuwa hivyo.

Hii ni mara ya pili Zahera akimlalamikia Nyika na mara ya kwanza alilamika hadharani kuhusiana na suala la mambo kutokwenda kwa mpangilio.


6 COMMENTS:

  1. Ndio maana hawatak uchaguz mafarasi hao

    ReplyDelete
  2. Ombi la kutaka wachezaji kukipa nguvu kokosi hazikutekelezwa ni miongoni ya mambo yaliyomkera na kutaja kujiondoa

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. Hivi lakini si ndo huyu huyu alizuia usajili kisa kuna wachezaji wengi wanaidai timu fedha za mishahara na za usajili, tena leo analalamika nini jamani!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic