Mshambuliaji wa zamani wa Mgambo JKT, Yanga na Lipuli ambaye kwa sasa anakipiga katika kikosi cha Arusha United kinachoshiriki Ligi daraja la kwanza, Malimi Busungu amesema kuwa wanaomponda kuwa ni mlevi hawana jipya.
Busungu aliachana na Lipuli ambayo inashiriki Ligi Kuu Bara kwa kile alichoeleza kuwa anadai stahiki zake kwa viongozi hali iliyomfanya asiwe na amani na kuamua kujiweka kando na sasa ameibuka akiwa ni mchezaji wa Arusha United.
"Kuhusu kulewa hakuna mwenye uhakika na hilo, kuna tofauti kati ya mlevi na yule anayekunywa ila huwa nafanya hivyo baada ya kumaliza kazi na sio wakati wa kazi najitambua na jukumu langu la kucheza mpira ndilo nalipa kipaumbele.
"Suala la mimi kuitwa mlevi, sina nidhamu hilo halina mahusiano kabisa na kile ambacho ninakifanya uwanjani, nina uwezo mkubwa na kipaji changu ni asilia hivyo maneno hayawezi kunipoteza kwenye ramani," alisema.
Arusha United ipo chini ya Kocha Felix Minziro ambaye alifanikiwa kuzipandisha Ligi Kuu Singida United na KMC ambazo zote zipo ligi kuu kwa sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment