January 22, 2019






Mshambuliaji mpya wa Cardiff City, Emiliano Sala anahofiwa kufariki kwenye ajali ya ndege.

Polisi ya Ufaransa imethibitisha kwmba Sala ambaye alitua Cardiff baada ya KRC Genk kukataa kumuuza mshambuliaji wake, Mbwana Samatta alikuwa kwenye ndege hiyo.

Ndege hiyo ilitoweka kwenye rada karibu na kilicho jirani na Wales.

Imeelezwa ndege aliyokuwamo ilikuwa njiani kwenda Cardiff na Sala alikuw amejipanga kuanza kazi yake hiyo mpya.

Baada ya kusaini mkataba kwa kitita cha pauni milioni 15, Sala alirejea Nantes nchini Ufaransa na kuwaaga wachezaji wenzake huku akikamilisha masuala kadhaa ya kifamilia.


Ujumbe wake wa mwisho kwenye Mtandao wa Kijamii wa Twitter, aliwaaga wote waliokuwa pamoja, kumuunga mkono na kadhalika kwa kuwa alikuwa anakwenda kuanza kazi mpya.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic