Mlinda mlango namba moja wa Yanga, Klaus Kindoki amekubali kuokota mipira mara tatu nyuma ya nyavu katika mchezo wa michuano ya SportPesa Cup ambao umechezwa Uwanja wa Taifa
Yanga imecheza na KK Sharks ya Kenya na tayari Kindoki amegeuka mara tatu baada ya kuanza mapema dakika ya 12 kupitia kwa Abuye Duke na kugeuka tena dakika ya 36 kupitia kwa Abege George.
KK Sharks walirejea kipindi cha pili wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0 ambayo waliyapata katika kipindi cha kwanza baada ya kushambulia.
Kipindi cha pili dakika ya 87 Yanga walifunga bao la kufutia machozi kupitia kwa Amiss Tambwe hali iliyoamsha ari kwa KK Shark kufunga bao la tatu dakika ya 90 kupitia kwa Abuye Duke.
Lakini Yanga waliamka na kufunga bao la pili ndani ya dakika za lala salama kupitia kwa Herieter Makambo.
Kesho ni zamu ya Simba kumenyana na AFC Leopards Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 na Mbao watafungua dimba saa 8:00 mchana kwa kumenyana na mabingwa watetezi Gor Mahia.
Eti Zahera atachukua makombe yote! Hata FA cup asahau..nadhani baada ya kipigo cha Stand united na hiki atajua mpira hauchezwi kwa maneno. Kuna makocha hapa Tanzania hawaongei ongei
ReplyDeleteKama kocha Babu Hans Plujim haongei
DeleteWalisusa kupeleka kikosi cha kwanza kujiandaa na Ligi kuu pamoja na Sportpesa,lakini waaapi,vipigo vinawaandama. Hahahahahahaaa
ReplyDeleteNa mambo bado....wakichomoa hizo mechi tano za ugenini...hongera yao
ReplyDeleteKwa hiyo saleh jembe hayo ndiyo matokea mnatupatia kwa kichwa cha habari hicho? Si na Singida United mgeaandika hivyo hivyo? Au kwa kuwa timu yenu imefungwa
ReplyDelete