January 12, 2019


Al Ahly ya Misri inakuja Dar es Salaam wikichache zijazo na mchezaji wa ajabu. Kwa lugha za mtaani unaeza kusema ni mchezaji wa kufuru. Yaani gharama yake inasajili vikosi vyote vya Ligi Kuu Bara na chenji inabaki. Kikosi kizima cha Simba ni Sh 1.3 Bilioni.

Yaani hapo unajumuisha watu kama Cletus Chama,Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Jonas Mkude, Aishi Manula. Usisahau kina Erasto Nyoni, James Kotei, Said Ndemla, Shiza Kichuya, Adam Saramba,Paschal Wawa, Shomari Kapombe na wengine kibaoo… ambao wanatamba Msimbazi.

Sasa Al Ahly ya Misri ambayo ipo kundi moja na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika imesajili winga matata Hussein El-Shahat kutoka Al Ain ya Falme za Kiarabu (UAE)kwa thamani ya Sh11.5 Bilioni. Piga hesabu hapo uone anaingia mara ngapi katika kikosi cha Simba, haipungui mara 10 tena na chenji inabaki nyingi tu.

Ndiye mchezaji ghali zaidi klabuni hapo na imemsajili kutoka kwenye klabu ya Ain ya Falme za Kiarabu. Mchezaji huyo ni raia wa Misri ambaye amecheza soka la kulipwa miaka mingi.

Ahly ambao lengo la kuhakikisha wanafanya maajabu kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, wameshamalizana na mchezaji huyo mwenye miaka 26 ambaye Ligi Kuu ya UAE alipachika mabao 15 msimu huu na kutoa asisti 17 katika michezo 33 ya mashindano yote.

2 COMMENTS:

  1. Ahly wanajeuri ya fedha sio mchezo. Huyu mchezaji wamemnunua kwa thamani ya dollar million tano na kitu. Lakini wameajiri kocha kutoka Uruguay na wengine kadhaa wa viwango vya juu kwa kweli hawa jamaa wamekusudia hasa sio mchezo.

    ReplyDelete
  2. Mbona hao Ahly wanapigwa tu huku na timu za Saudi Arabia na za Emirates !!!
    Tatizo timu za Bongo zinawaogopa na timu za huku haziwaogopi. Niwape mbinu ukitaka mmisry asicheze mpira muudhi kwa maneno anakasirika haraka na kutoka katika mood ya kucheza !! Wafundisheni wachezaji baadhibya maneno ya kuwadharau!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic