KIKOSI cha Mtibwa Sugar kimeshindwa kupata pointi pamoja na bao katika michezo yake mitatu mfululizo waliyocheza ambayo ni sawa na dakika 270 ya Ligi Kuu Bara kwa kuambulia kipigo.
Kocha Mkuu wa Mtibwa, Zuber Katwila amesema kikubwa kinachowafanya washindwe kupata matokeo ni safu yake ya ushambuliaji kushindwa kuwa makini wakiwa eneo la hatari.
"Wachezaji wangu wanacheza vizuri na wanatengeneza nafasi nyingi katika michezo yetu ila kinachotukwamisha ni kukosa umakini kwa safu yangu ya ushambuliaji jambo ambalo limenifanya nikae chini na wachezaji wangu kutafuta mbinu mpya kulitibu tatizo.
"Ushindani ni mkubwa kwenye ligi na kupoteza mchezo haina maana ya kushindwa kuhimili mikikimikiki, imani yangu bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kupata matokeo kwenye michezo yetu inayofuata kikubwa sapoti kwa mashabiki," alisema Katwila.
Mtibwa Sugar wamepoteza michezo hiyo kwa kwa kuanza mbele ya Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 kisha Mbeya City bao 1-0 zote Uwanja wa Sokoine na hivi karibuni wamepoteza mbele ya Lipuli kwa bao 1-0 Uwanja wa Manungu.
0 COMMENTS:
Post a Comment