KIKOSI cha Simba Queens leo kitakuwa kazini kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake maarufu kama Serengeti Lite Women's Premier League dhidi ya Baobab mkoani Dodoma.
Simba Queens ambao kwa sasa wamecheza michezo sita na kufanikiwa kushinda michezo minne na kutoa sare moja pamoja na kupoteza mmoja wanakutana na Baobab ambayo imepoteza michezo mitano na kushinda mchezo mmoja.
Kocha wa Simba Queens, Omary Mbweze amesema wamejipanga kiasi cha kutosha kuibuka na pointi tatu kutoka makao makuu ya nchi.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu ni timu bora ambayo inapambana ila hilo halitupi hofu kutokana na maandalizi tuliyoyafanya.
"Hesabu zetu ni kuona tunabeba pointi tatu ili tujiweke katika nafasi nzuri ya ushindani, kila timu ina malengo ambayo imejiwekea hivyo ili nasi tufikie malengo yetu kuna haja ya kupata matokeo leo," alisema Mbweze.
0 COMMENTS:
Post a Comment