January 12, 2019


IKIWA leo Simba wanashuka Uwanjani kuiwakilisha nchi katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura na kuikosa huduma ya beki kiraka Erasto Nyoni, beki huyo amewatumia ujumbe mashabiki wake.

Nyoni aliumia katika goti alipokuwa akitumikia timu yake kwenye mchezo wa kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM visiwani Zanzibar kwa sasa yupo chini ya uangalizi wa jopo la madaktari ili arejee kwenye ubora wake.

Nyoni amesema hakuna haja ya mashabiki kuwa na hofu naye wala kikosi chake cha Simba kwani anawamini wachezaji na wanatambua wamebeba furaha ya mashabiki na taifa kiujumla.

"Namshukuru Mungu kwa sasa naedelea vizuri hivyo kikubwa tu ni mashabiki kuwa na timu yetu bega kwa bega, kwenye michezo mengi yanatokea ila uhakika wa kufanya vizuri kwa wachezaji upo na watapeperusha vema bendera ya Taifa," alisema Nyoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic