ILE HAZINA YA YANGA SASA YAGEUKA KUWA LULU AZAM
Straika wa Azam FC, Donald Ngoma, amesema kwamba kocha wake, Hans van Der Pluijm, ni mtu ambaye anamuelewa vizuri jinsi ya kumtumia, anamuelekeza vizuri na anamuelewa pale anapokuwa kazini.
Kwa mujibu wa Championi Ijumaa baada ya mchezo wao dhidi ya Malindi ambapo Azam ilishinda kwa mabao 2-1 katika Mapinduzi Cup, alisema anajisikia furaha kuitumikia timu hiyo kwani amekuwa akimpa mbinu ambazo zinaeleweka na kumfanya kuwa imara zaidi.
“Ananielewa vizuri, kwa kuwa tulishawahi kufanya kazi pamoja huko nyuma, hiyo inanisaidia kuzoea mazingira ya Azam FC na ninaamini nitafanya vizuri,” alisema Ngoma.
Kuhusu hali ya hewa ya Zanzibar, Ngoma alisema ni nzuri na anaifurahia na kuweka wazi kuwa yeye anapendelea kula ugali nyama au ugali kuku.
Ngoma na Pluijm waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Yanga.
Azam FC imeingia nusu fainali ya Mapinduzi Cup ambapo inatarajiwa kucheza dhidi ya Mlandege leo Ijumaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment