January 22, 2019


KIKOSI cha Mbao FC kitakuwa kazini kesho kumenyana na Mabingwa watetezi wa kombe la SportPesa Gor Mahia katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Wabishi hao kutoka Mwanza ni mara yao ya kwanza kushiriki michuano hii ambayo msimu huu yanafanyika Dar es Salaam, mtihani wao wa kwanza utakuwa mbele ya Gor Mahia kesho majira ya saa 8:00 mchana.

Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njash amesema kuwa wanatambua thamani ya kualikwa kwenye michuano hii ya kimataifa hali itakayowafanya waonyeshe ushindani wa kweli.

Mchezo wa pili utakuwa ni kati ya Simba na AFC Leopards Uwanja wa Taifa utakaochezwa saa 10:00 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic