Waamuzi wa mchezo kati ya JKT Tanzania na Simba uliopigwa katika Uwanja wa Mkwakawani, Tanga, Mbaraka Rashid amepewa onyo kali kutokana na kutokuwa makini huku msaidizi wake, Mashaka Mwandembwa akifungiwa miezi mitatu.
Wakati waamuzi hao wakikumbana na hilo, wachezaji wa Singida United, Geofrey Mwashiuya na Rajabu Zahiri wamefungiwa mechi tatu kila mmoja.
Adhabu hizo na mashauri mengine yamefanywa baada ya Kamati ya Uendeshaji ya Ligi kupitia malalamiko na matukio tofauti ambayo yalitokea katika mechi tofauti za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, hivi karibuni.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura amesema: "JKT walileta malalamiko yao juu ya mchezo wao na Simba.
“Malalamiko yamepitiwa na mwamuzi wa mchezo ule Mbaraka Rashid amepewa onyo kali kutokana na kutokuwa makini lakini msaidizi wake Mashaka Mwandembwa amefungiwa miezi mitatu kutokana kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea 'offside'.
"Wachezaji wa Singida United, Geofrey Mwashiuya amefungiwa mechi tatu baada ya kumpiga mchezaji wa Biashara United huku Rajab Zahiri katika mchezo huohuo alitaka kumpiga mwamuzi, hivyo kafungiwa mechi tatu na kocha wao Shadrack Nsajigwa amefungiwa mechi mbili na faini ya Sh 500,000 kutokana na kujibizana na mwamuzi.
"Singida wamepigwa faina ya Sh 200,000 baada ya kushindwa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo na kwenda chumba cha waandishi wa habari walipocheza na Simba. Pia mtunza vifaa wa Ruvu Shooting, Augustine Kalangwa, amepelekwa katika Kamati ya Nidhamu.
"Mbao FC na Alliance zimepigwa faini Sh 500,000 baada ya kushindwa kuingiza timu za U-20 zilipokutana na Kocha wa Makipa wa Lyon, Juma Bomba amefungiwa mechi mbili na faini ya Sh 500,000 baada ya kumjibu vibaya mwamuzi.
"Kocha wa Kitayosce, Hamad Haule amefungiwa mechi mbili na faini ya Sh 500,000 baada ya kutumia simu akiwa kwenye benchi tukio lilitokea kwenye mechi ya Kitayosce na Kilimanjaro," alisema Wambura.
Maamuzi ya ajabu na kijinga.Hiyo kamati inakuwa kipofu wanapojadili timu moja lakini wana macho sita inapohusisha timu ndogo. Mchezaji anampiga mwenzake kichwa wazi wazi kabisa hapewi adhabu yeyote zaidi ya kukosa mechi.Wengine wakapigwa faini na kukosa mechi.Waandishi wapo kimya kwa sababu haiathiri timu yao.
ReplyDeleteKuna kocha alionekana Mbeya akibishana na waamuzi kwa fujo tena bila hatua kuchukuliwa.
Refa wa Yanga na Prisons aliyepigwa na wachezaji Makambo na Andrew Chifupa hakuchukua hatua wala kuchukuliwa hatua eti hamna ushahidi.
Give me a break!
Halafu tunategemea maendeleo ya mpira.
Ushahidi wa matukio hayo upo wazi Azam Tv.
Nadhan umetazamia upande mmoja... lakin kumpa mtu au mchezaji adhabu unaangalia source of that miss leading na ndo unatoa adhabu usiangalie outcome ndo utoe adhabu
DeleteUsipanic shida bongo kati ya SIMBA NA YANGA wa timu flan ikiadhibiwa au ikiachiwa UPANDE WA PILI WANALAUMU
WAKAT watu wamekaa chini na wakapembua whats good en whats wrong within a certain circumstance
SAMAHAN KAMA NMEKUKERA
Uko sawa kabisa kama hajakuelewa akae chini
DeleteHapa suala sio upande wa pili.Hapa ni Justine.
ReplyDeleteKuna Maemo maarufu kuhusu haki.Justice should not only be done but must be seen to be done.
Huwezi kuadhibu wachezaji waliofanya makosa makubwa ukawaacha wengine.
Angalia kwa wenzetu ingawa sio perfect lakini haki inafanya kazi.
Nafikiri uliona mpira wa Yanga na Mwadui tarehe 15 mwezi huu.
I rest my case.