January 19, 2019





Kiungo wa Simba, Claytous Chama, ameizungumzia AS Vita Club kuwa ni timu ngumu, lakini watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo wao wa leo Jumamosi.


Chama ambaye tangu hatua ya awali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika amekuwa akiisaidia kwa kiasi kikubwa timu yake ya Simba, leo Jumamosi anatarajiwa kuwa kwenye kikosi ambacho kitapambana na AS Vita Club ukiwa ni mchezo wa michuano hiyo, hatua ya makundi.


Katika mchezo huo ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Martyrs uliopo hapa Kinshasa nchini DR Congo, Simba inatakiwa kuhakikisha haipotezi ili kujiweka vizuri kwenye kundi lake la D ambalo kwa sasa inaongoza ikiwa na pointi tatu.
Chama ambaye ni kati ya wachezaji 19 waliotua jijini hapa Alhamisi kwa ajili ya mechi hiyo, alisema: “Mechi itakuwa ngumu kutokana na wapinzani wetu kuwa nyumbani kwao, lakini licha ya sisi kuwa ugenini, hatutakuwa wanyonge.


“Tupo tayari kwa vita, tutapambana nao mwanzo mwisho kuhakikisha hatupotezi mchezo huu, tumedhamiria kufika mbali, hivyo ni lazima kulinda kila pointi kwenye mechi zetu.


“Niseme tu, kwa muda ambao tumekaa huku DR Congo, tayari tumezoea hali ya hewa na mazingira yake, hivyo tupo vizuri.”


Simba ilitua hapa DR Congo juzi Alhamisi na inatarajiwa kurejea Tanzania kesho Jumapili baada ya mchezo huo kuchezwa leo Jumamosi.

1 COMMENTS:

  1. Waandishi wa blog hii, muwe watafutaji wa habari na wafuatiliaji wa habari za michezo kila wakati na kuweza kutoa taarifa muafaka kwa wakati sahihi, sio kusubiri hadi magazeti yatoke ndipo nanyi mchukue habari kwenye magazeti ndio mtuwekee humu, tumieni resources zenu kupata taarifa muhimu kwa wakati.
    mfano, kwasasa Timu yangu ya Simba haioongozi, kwani jana usiku kuna mchezo wa kundi hili "D" ulichezwa kati ya Al Ahly na Saoura na wametoka sare ya bila kufungana. Hivyo hadi sasa Ahly anaongoza kwa point 4 na Simba inafuatia ikiwa na point 3. Tunazidi kuiombea Simba ipate matokeo leo ili iendelee kuongoza.
    Kwahiyo, kuweni watafutaji wa taarifa za michezo kwa wakati. Ina maana hata kuuangalia mpira usiku mmeshindwa! basi hata kuuliza tu asubuhi kwa walioangalia matokeo yalikuwaje! Hadi mngoje Championi litoke ndio nanyi mkopi na kupest!.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic