MABINGWA wa kihistoria wa kombe la Ligi Kuu Bara Yanga wameonekana kushindwa ujanja wao wa kuendeleza rekodi za kutoruhusu kufungwa nje ya mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya kuishia kanda ya Ziwa.
Yanga msimu uliopita wa mwaka 2017/18 mchezo wao wa kwanza walipoteza mbele ya Mbao FC, Uwanja wa CCM Kirumba kwa kufungwa mabao 2-0 na msimu huu pia wamepoteza mchezo wao wa kwanza kanda ya Ziwa mbele ya kikosi cha Stand United.
Yanga ilifanikiwa kucheza michezo 19 bila ya kupoteza zaidi ya kushinda michezo 17 na kutoa sare michezo miwili Ilipoteza mchezo wake wa kwanza mbele ya Stand United Uwanja wa CCM Kambarage.
Bao pekee lililofungwa na Jacob Massawe dakika ya 88 limetosha kutibua rekodi ya mabingwa hao na kushindwa kuendeleza ubabe wao wakiwa kanda ya Ziwa na kuruhusu Stand United kuvunja mwiko wa kutofungwa.
Licha ya kupoteza mchezo huo bado wanashika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 53 huku wapinzani wao Simba wakiwa nafasi ya nne na pointi zao 33 huku nao pia mchezo wao wa kwanza msimu huu walipoteza kanda ya ziwa mbele ya Mbao FC kwa kufungwa bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment