UONGOZI wa Simba umeshangazwa na tabia za mashabiki kuwalaumu viongozi baada ya kupoteza mchezo wa jana wa SportPesa Cup hatua ya nusu fainali kwa kufungwa bao 2-1 na Bandari ya Kenya.
Simba jana ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya SportPesa na kuyeyusha mipango ya kucheza na Everton ya England pamoja na kupishana na fuko la fedha za mshindi wa kwanza zaisi ya milioni 60.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema mashabiki wa Simba na watani zao wamekuwa wakiwasema kwa maneno mazito ambayo si ya kiungwana hali ambayo kishabiki haina maana.
"Wengi wananivaa mimi na kunipa lawama ambazo sistahili kisa tumefungwa, mashabiki wanapaswa watambue kuwa mimi si mchezaji, siwezi kufunga kazi yangu kubwa ni kuhamasisha mashabiki pamoja na wachezaji kucheza kwa morali.
"Wanalalamika mara Niyonzima amekosa nafasi ya wazi mnataka mimi nifunge? Okwi ameshindwa kufunga mimi nifanye nini, najua tumefungwa michuano ya SportPesa Cup tunashindwa kucheza na Everton ila lawama na matusi tunashushiwa viongozi, mashabiki tubadilike ," alisema Manara.
Sasa alaumike nani wakat mnafanya utumbo adi sasa tushakosa makombe 3 mwaka huu tutakosa yote na yalobak
ReplyDeleteHata viongozi mnatakiwa kumuangalia kocha Aussen patrick kwa jicho pevu na yakinifu kwani anaonekana hana mbinu mbadala hasa timu inapoelemewa,anapenda majaribio,hana ushirikiano kwa benchi la ufundi,anapenda kujiamulia,matendo 12 ya awali kama vile,kujumlisha,kutoa,kuzidisha na kugawanya yanamshinda,amekariri mfumo,anapenda kujilinda sana.Mwisho Kocha anakoelekea hata majukumu ya kamati ya ufundi(kuloga mechi)itafikia hatua atataka aloge yeye badala ya mashabiki mzee wa Uchebe ni wazi kuwa ni Mhuni anamwanzisha nje dilunga anaanza na muzamiru matokeo yake timu inakuja kuonekana wachezaji wote wanachezea zone ya goli letu.Viongozi watambue kuwa Mzee wa uchebe ni mbinafsi ambaye hashauriki Masoud Ilambona Djumaa atabaki kuwa mwalimu bora hata kama viongozi walimtoa kwa mahaba yao na Mzee wa Uchebe
ReplyDeleteUlisema simba level yake man city,Barcelona na Bayern ndio maana watu wanakuhukumu
ReplyDeleteJIUZULU KAMA UNAONA HUNA NAFASI YA KULAUMIWA WEWE NI KIONGOZI MASHABIKI WANA MWISHO WA KUWAVUMILIENI MNAWARUHUSU WACHEZAJI WANAENDA KULEWA WANAACHA KAMBI KESHO YAKE TUNAFUNGWA MNADHANI HATUJUI? SIMBA INAKUWA LEGELEGE KILA SIKU KOCHA KARELAKSI MAMBO YA OVYO WATU HUKU WANAZIMIA KWAAJILI YA MATOKEO MABAYA SIMBA GANI HII HAIFUNGI MAGOLI WANASHINDWA KUWAFUNDISHA SHABAHA WACHEZAJI MWAKA MZIMA? MASHUTI HUYAONI KAZI KUCHENGA TUUU
ReplyDeleteNIWAAMBIE UKWELI VIONGOZI SIMBA, NENDENI CONGO KUNA MAKOCHA WAZURI KULIKO HUYU MZUNGU UNATUCHEZEA AKILI ZETU. CONGO WAPO MAKOCHA WATATUSAIDIA SIMBA KWA GHARAMA NAFUUU
DeleteHuyu kocha ameshafeli. Kuna makocha wazuri sana na kwa bei chee kutoka Serbia, Croatia, Romania, Bulgaria.Mnawakumbuka kina Circovic, Kuponovik,Samsorov,Popadic,ambaye ameanza kuinoa Singida United.Viongozi tafakarini
DeleteMasoud Juma alikuwa mzuri kuliko huyu mzee. Ndiyo sababu mzee alimfukuzisha simba kwa sababu hapendi ushindani. Simba itapata shida sana mwaka huu. Bado vichapo kama vinne hivi kwenye ligi kama isipofanya marekebisho kwenye bench la ufundi. Wasikazanie kwenda kusajili wachezaji wa mabilioni kutoka nje wawape akina kichuya na wazawa nafasi na watafute Kocha Mzuri.
ReplyDeleteAdui namba moja wa Mikia ni huyu Manara. Yaani anawajaza ujinga mashabiki wakati timu ina kiwango cha kawaida tu...
ReplyDelete