KIKOSI cha Simba kinafanikiwa kutinga fainali baada ya kushinda mchezo wa nusu fainali ya pili ya kombe la fainali kati ya Simba na Malindi SC, mchezo uliochezwa Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.
Dakika tisini zilikamilika bila timu hizo mbili kuweza kupata nafasi ya kuona lango la mpinzani hali iliyofanya kuweza kupelekea kwenye matuta ili kumpata mshindi atakayekutana na Azam FC ambaye leo alishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya KMKM.
Katika mamuzi ya penati Simba walifanikiwa kushinda kwa mabao 3-1 baada ya penati hizo kupigwa, wafungaji kwa upande wa Simba walikuwa ni Yusuphu Mlipili ambaye alikuwa ni nahodha wa timu, Mohamed Ibrahim na Asante kwasi huku beki Zana Coulibary akikosa penati kwa upande wa Simba.
Kwa upande wa Malindi, aliyepata penalti alikuwa ni Abdul Kassim huku Ally Juma Mabata, Mwalami Issa shuti lake likipanguliwa na Ally Mustafa na Aly Chollo alipaisha penalti yake ya mwisho na kuifanya Simba ifanikiwe kupenya hatua ya fainali ya kombe la Mapinduzi.
This is simbaaaaaaa
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteWe Can, This is Simbaaaaaaaa
ReplyDelete