January 13, 2019


Na George Mganga

Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, amemwaga pongezi za dhati kwa Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Muro ameeleza kuwa hatua waliyofikia Simba imewatoa kimasomaso watanzania wote baada ya ushindi huo.

Aidha, Muro amempongeza Msemaji wa Simba, Haji Manara kwa namna anavyojitoa kutia hamasa na morali kwa mashabiki wa Simba na kuwa sababu au chachu ya matokeo mazuri.

Muro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, ameeleza hayo katika ukurasa wake wa Instagram kwa kumwaga pongezi hizo kwa Simba.

"Tuna kila sababu ya kusimama pamoja kama taifa na kuipongeza sana Simba, hakika mmetutoa kimasasomaso watanzania, ndugu yangu Haji Manara hongera, hamasa yako imekuwa chachu ya matokeo mazuri uwanjani. This Is Amazing And Fantastic" - Jerry Muro (Mkuu wa Wilaya ya Arumeru)

7 COMMENTS:

  1. huyu mnafiki sana tena mshe zi amewahisema simba haitafika popote leo analeta unafiki wake mp u xxz sana huyu apeleke unafiki hukoo

    ReplyDelete
  2. Hata mimi namshangaa leo, Huyu na Mwenzake Ridhiwani, majuzi tu walisema Simba isilewe sifa, haiwezi kufika popote, mara viingilio vya laki cjui vimefanya nn! Leo hii wanaipongeza. ni kufuta aibu tu huko, hakuna lolote.

    ReplyDelete
  3. Simba inaweza bhana! hilo lazima tulikubali. Hata wale jamaa zetu wa upande wa pili jana walikuja Taifa wakiwa na mabango yameandikwa "NO YOU CANT, SAOURA IS KISIKI CHA MPINGO", wale jamaa hata sikuwaona tena na bango lao! sijui walitokea mlango gani! nadhani hata kujuta walijuta juu ya muda na gharama walizotumia kuliandika bango lile!. Itawabidi mpende tu sasa, soka safi mmeliona tena la burudani, na bado magoli mmeyaona yote ni magoli ya akili na ya mateso makubwa kwa wapinzani. kubalini tu jamani.

    ReplyDelete
  4. TFF ijitathmini namna inavyoendesha soka la Tanzania....kwani kumekuwa na malalamiko ya upendeleo na kuzipangia unafuu ratiba ya mashindano baadhi ya klabu fulani na kuzikandamiza nyingine....sijata timu hizo ila mwenye macho haambiwi tazama

    ReplyDelete
  5. mimi ni shabiki wa yanga ninayeishi nchi za kiarabu kusema kweli hii tabia ya kushangilia timu pinzani zinapokuja kucheza Tanzania hua zinaniudhi sana na hii ni tabia ya washangiliaji wa timu zote mbili SIMBA na YANGA kwa hiyo muache ushamba huo NA SI UZALENDO maana hapa tunachekwa sana na wamisry na mataifa mengine kwa kufanya kitendo kama hicho ambacho huwezi kukiona kwa timu za wenzetu. HAPA TIMU YOYOTE YA WATANZANIA INAPOFUNGWA TUNAOZOMEWA NI SISI WATANZANIA SABABU HAO NI WAWAKILISHI WA TANZANIA

    ReplyDelete
  6. Hongereni sana simba
    By Ally Baba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic