Uongozi wa klabu ya Simba umesema awamu hii una malengo ya kuchukua taji la SportPesa Super Cup inayoataraji kuanza leo katika jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, amesema wamejipanga vilivyo kuhakikisha kikombe hicho kinabaki nchini ili wapate nafasi ya kucheza na Everton.
Manara amesema wao kama klabu wanajua namna gani wanachama na wapenzi wa Simba walivyosikitishwa na kipigo walichokipata dhidi ya AS Vita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo wamedhamiria kuwasahaulisha kwa kufanya vema kwenye mashindano ya SportPesa.
"Unajua wapenzi na wanachama wetu wengi wameumiza na matokeo ya kufungwa mabao 5-0 na AS Vita, tuna mpango wa dhati kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye SportPesa CUP ili tuweze kuchukua kikombe na kuwapa faraja wapenzi mashabiki zetu" alisema.
Wakati yanga ikianza kibarua chake kwa kucheza na Kariobang Sharks ya Kenya leo, kesho Simba watakuwa watakuwa wanakipiga na AFC Leopards kutoka Kenya pia.
0 COMMENTS:
Post a Comment