KISA STAND UNITED, VIONGOZI YANGA WATAKIWA KUWANUNULIA WACHEZAJI VIATU VYA MAANA
Na George Mganga
Kitendo cha timu ya Yanga kufungwa bao 1-0 na Stand United kisha kuvunja rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote msimu huu kimemuibua Mwanachama wa klabu hiyo, Edgar Chibula kwa kuutaka uongozi ununue zana za kazi.
Chibula ambaye ni shabiki lialia wa Yanga, ameutaka uongozi wa Yanga kuwanunulia viatu wachezaji wake ambavyo vinaendana na hali hewa ilivyo kwa sasa.
Akizungumza kupitia Radio One, Chibula amesema kipindi hiki kuna mvua hivyo inawezekana Yanga ikashindwa kupata matokeo kama ilivyokuwa kule Shinyanga.
Chibula anaamini kuwa Yanga ilishindwa kung'ara Shinyanga baada ya mvua kunyesha na kusababisha wachezaji kushindwa kuhimili mikikimikiki ya uwanjani.
Amevitaja viatu ambavyo walikuwa wakitumia pengine vinashindwa kuendana na hali ya mvua hivyo ni vema kama waajiri wakawanunulia vingine ili viwasaidie.
"Ni vema uongozi ukaangalia upya suala la viwanja na hali ya hewa kuwa na mvua kipindi hiki, nawaomba wafanye mpango wa kuwanunulia wachezaji viatu vya maana ili waweze kuendana na mikikimikiki ya uwanjani" alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment