January 13, 2019


Kocha Mkuu wa JS Saoure ya Algeria, Nabil Neghiz amesema kilichowaponza wakashindwa kuibuka na ushindi mbele ya Simba ni ugeni wa mashindano ya kimataifa.

Neghiz alikuwa Uwanja wa Taifa akiiwaongoza waarabu hao wakiwa na mytanzania Thomas Ulimwengu kutafuta ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kimataifa ambao wamekubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0.

Neghiz amesema, Simba sio timu ya kubeza na alikuwa anatambua hilo awali hali iliyomfanya awape mbinu wachezaji wake ila bahati haikuwa upande wake kutokana na maamuzi pamoja na ugeni wao wakapoteza.

"Naitambua Simba ni timu ngumu, ina wachezaji wenye uzoefu na mashindano ya kimataifa tofauti na timu yangu, ila licha ya ubora wao tumeonyesha nasi tunaweza hivyo ni wakati wao kujitahidi kuwa bora zaidi.

"Katika namna nyingine mwamuzi aliwabeba Simba kwani bao la pili halikuwa sawa ila ndo imetokea tumepoteza tuna nafasi ya kujipanga na tumeonyesha kwamba sisi sio timu dhaifu," alisema.

2 COMMENTS:

  1. Mashabiki wa Yanga mnaidhalilisha nchi kushangilia wageni ni mara mia bora mkaae nyumbani kuliko kuja uwanjani na kushangilia mwishoni aibu inawakuta Simba itashinda tu....huu ni mkakati (TFF, Simba wanachama, wageni, Serikali kuu, serikali ya mkoa na Jeshi la Polisi na wadhamini au wawekezaji wa klabu ya Simba) pointi 9....kwa mchina lazima....nguvu moja....ni kauli mbiu kwa vitendo....

    ReplyDelete
  2. Simba inaweza bhana! hilo lazima tulikubali. Hata wale jamaa zetu wa upande wa pili jana walikuja Taifa wakiwa na mabango yameandikwa "NO YOU CANT, SAOURA IS KISIKI CHA MPINGO", wale jamaa hata sikuwaona tena na bango lao! sijui walitokea mlango gani! nadhani hata kujuta walijuta juu ya muda na gharama walizotumia kuliandika bango lile!. Itawabidi mpende tu sasa, soka safi mmeliona tena la burudani, na bado magoli mmeyaona yote ni magoli ya akili na ya mateso makubwa kwa wapinzani. kubalini tu jamani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic