January 13, 2019


Straika Mtanzania abayekipiga katika klabu ya JS Saoura, Thomas Ulimwengu amesema Simba wametumia faida ya Uwanja wao wa nyumbani kupata matokeo.

Ulimwengu ambaye amejiunga na timu hiyo hivi karibuni, ameeleza walizidwa mchezo huo na faida ya uwanja wa nyumbani imeapa Simba matokeo.

Katika mchezo ambao Saoura walikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba, ulionekana zaidi kuwa wa upande mmoja baada ya waarabu kuzidiwa kwa kila kitu.

Licha ya matokeo hayo, Ulimwengu amefunguka kuwa nao watajipanga vema katika mechi inayofuata ili kumalizana na Simba vizuri.

Ulimwengu ameweka rekodi ya kucheza mchezo huo wa kwanza huku timu yake ikipoteza kwa mabao 3-0.

1 COMMENTS:

  1. Mashabiki wa Yanga mnaidhalilisha nchi kushangilia wageni ni mara mia bora mkaae nyumbani kuliko kuja uwanjani na kushangilia mwishoni aibu inawakuta Simba itashinda tu....huu ni mkakati (TFF, Simba wanachama, wageni, Serikali kuu, serikali ya mkoa na Jeshi la Polisi na wadhamini au wawekezaji wa klabu ya Simba) pointi 9....kwa mchina lazima....nguvu moja....ni kauli mbiu kwa vitendo....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic