KOCHA Mkuu wa Bandari, Bernard Mwalala amesema kikosi chake kimefanya kazi kubwa licha ya kushindwa kutwaa ubingwa wa SportPesa Cup jana mbele ya KK Sharks bado nao ni mabingwa katika mashindano.
Bandari walipoteza mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa kwa kufungwa bao 1-0 dakika ya 60 na Mwendwa Harrison lililodumu mpaka mwisho wa kipindi.
Mwalala amesema licha ya kushindwa kutwaa kombe bado kikosi chake ni imara kilichowaponza wafungwe ni kuzidiwa maarifa na mpinzani wake.
"Tunatoka wote nchi moja na tunashiriki ligi moja, timu zote mbili ni bora, mpaka sasa kwenye ligi mimi sijafungwa na mwenzangu pia hajafungwa hivyo unaona namna ilivyo ngumu kupata matokeo.
"Tumecheza michezo mitatu yote naona tumeshinda na ni washindi licha ya kushindwa kutwaa kombe kwani ushindani ulikuwa mkubwa," alisema Mwalala.
0 COMMENTS:
Post a Comment