January 14, 2019




UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mpaka sasa kumekuwa na tatizo la mawasiliano kati ya mwalimu wa kikosi hicho Mwinyi Zahera dhidi ya mshambuliaji Herieter Makambo kwa kuwa amekuwa hapatikani kwenye simu zake.

Makambo ambaye kwa sasa ni kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu Bara akiwa amefunga mabao 11 bado hajarejea kujiunga na timu hiyo ambayo kesho itacheza na Mwadui Uwanja wa Taifa.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema taarifa za uzushi ambazo zinasambazwa juu ya Makambo kwamba ameondoka Yanga hazina ukweli wowote zinapaswa zipuuzwe.

"Herieter Makambo alisafiri kwenda Congo, alisafiri kwa mapumziko mara baada ya mchezo dhidi ya Mbeya City kama ambavyo mwalimu alitoa mapumziko kwa wachezaji wengine, sio kweli kwamba ameondoka ndani ya timuila bado hatujaua ana tatizo gani alilolipata.

"Awali kulikuwa na mawasiliano kati ya mwalimu ambaye alikuwa anawasiliana naye siku zote, hata wakati anaondoka taarifa zilikuwepo kwa mwalimu ila kwa sasa kumekuwa na shida kidogo ya mawasiliano kati ya siku mbili, kati yake yeye Makambo na mwalimu," alisema Ten.

2 COMMENTS:

  1. Atapewa adhabu ya kuchelewa kuripoti kambini kama wachezaji wengine wanavyo adhibiwa?

    ReplyDelete
  2. Apewe adhabu na nani?
    Tshishimbi amepewa adhabu na nani?
    Kuna sheria mbili tofauti za wazawa na wageni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic