January 19, 2019



KOCHA wa Stand United, Amars Niyongabo amesema kikosi chake kimejiandaa kiasi cha kutosha kuvuruga kasi ya kinara wa ufungaji Ligi Kuu Bara, Herieter Makambo na kinara wa pasi za mwisho Ibrahim Ajibu kwa kuwawekea ulinzi imara Uwanjani.

Mshambuliaji Herieter Makambo wa Yanga ana mabao 11 mpaka sasa leo atakuwa mzigoni pamoja na nahodha wake mpya, Ibrahim Ajibu mwenye pasi 14 za mabao ndani ya Yanga.

Niyongabo amesema wanawatambua wapinzani wao vizuri hasa wachezaji wao muhimu ambao wanawategemea hivyo wamejipanga kuwadhibiti ili kupata ushindi.

"Tutakuwa nyumbani na tunatambua tunacheza na kikosi cha aina gani, huyo Ajibu ambaye wanamsifia kwamba ni fundi wa kupiga mipira iliyokufa ajipange kwani tumejipanga kupata matokeo.

"Kama wao wanamtegemea Makambo basi nasi tuna wachezaji wetu makini ambao watamzuia asipate matokeo hapa, waamuzi wazingatie kanuni 17 za mpira ili tusianze kutafutiana sababu," alisema Niyoganbo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic