REKODI zinambeba Kocha wa Simba, Patrick Aussems dhidi ya Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Congo na timu ya AS Vita Club Florent Ibenge ambayo itacheza leo na Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya Makundi.
Timu zote zimecheza michezo mitatu, miwili hatua ya awali na mmoja wa hatua ya makundi ambapo safu ya ushambuliaji ya Mbelgiji wa Simba imefanikiwa kufunga mabao mengi.
Katika mechi tatu ambazo Simba wamecheza wamefanikiwa kushinda michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja na wamefunga mabao saba.
Michezo hiyo ni dhidi ya Nkana FC Simba walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 ugenini na walipokutana nyumbani Simba ilishinda kwa mabao 3-1, mchezo wa kwanza wa Hatua ya Makundi Simba ilishinda mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura na kufanya safu ya ushambuliaji ya Simba kukusanya mabao saba mpaka sasa.
Safu ya Mcongo katika michezo mitatu imeshinda mchezo mmoja dhidi ya Bantu FC wakiwa nyumbani kwa ushindi wa mabao 4-1 na ule wa marudiano walitoka sare ya bao 1-1 na mchezo wao wa kwanza wa Hatua ya Makundi walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 na All Ahy na kufanya safu yake ya ushambuliaji kukusanya mabao matano mpaka sasa.
Simba atakuwa kazini leo kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa ukiwa ni mchezo wake wa pili na leo akiwa ugenini nchini Congo katika Uwanja wa Mertyrs.
Hizi sifa ndizo zinazoponza timu zetu
ReplyDelete