January 28, 2019


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amekanusha taarifa zinazoendelea kusambaa mtandaoni kwamba amewaita mashabiki wa Simba SC "wapumbavu" .

Manara amekanusha hilo huku akisema yeye alitumia neno "pumbavu" kwa wale waliokuwa wanamtusi yeye na mama yake kutokana na Simba SC kufungwa .

Msemaji huyo mwenye maneno mengi ameahidi sh million 5 kwa yeyote alitakayeweka video ikimuonesha akiwatukana mashabiki wa Simba SC.

Manara alifunguka kwa kusema hata ingekuwa nani ambaye amemtusia mama yake matusi ya nguoni kwasababu Simba imefungwa asingemwita jina zaidi ya mpumbavu.

2 COMMENTS:

  1. Dah! Kaka angu Manara, nakuamini sana wewe ni Jembe letu hapo klabuni, kwani unaisaidia sana Simba kwa ubunifu wako wa aina kwa aina katika kubuni hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa Simba na pia hamasa hiyo huhamia kwa wachezaji na hatimaye Simba kufanya vizuri na kuwa tishio kwa wapinzani.

    Ila safari hii kaka angu "umekanyaga waya". Sikumbuki ni siku gani ila ni mwezi huu wa kwanza, ulimpa ushauri mzuri sana MSEMAJI WA JIRANI ZETU WA YANGA, Ushauri ule niliupenda sana, hadi nami nika-comment humu ndani kuonyesha kuwa nimekukubali na kukuamini kuwa wewe ni msemaji uliyeingia katika nafasi hiyo ukiwa mkomavu.

    Ushauri huo ulitokana na Msemaji wa Yanga Bw. D. Ten kumtukana shabiki mmoja kwa kumwambia kuwa "aende akaangalie phonebook ya simu ya mama yake aone namba yake yaani ya Ten imeseviwa kwa jina gani". Ulimshauri vizuri saaaanaaaa, nikafurahi.

    Lakini na wewe leo umeshindwa kutuliza jazba zako na kuwaambia baadhi ya mashabiki waliokutukana kisa Simba yetu imefungwa, kuwa ni wapumbavu, na umesisitiza kuwa huna jina lingine la kuwaita zaidi mpumbavu!.

    Kaka, ushauri wako kwa wengine ni mzuri, mbona unashindwa kuufanyia kazi kwako?

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwa wewe aliyekutukana utamuita malaika, mpumbavu ni mkosefu mwenye kujua kile akifanyacho sasa hawa waliotukana hawajui walitendalo???

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic