January 28, 2019


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke, Lusubilo Mwakibibi ametoa siku 30 kwa wamiliki wa Uwanja wa Taifa, Sabasaba na Azam Complex kulipa ushuhuru wa huduma, imeelezwa.

Mwakibibi amesema wamiliki wa viwanja hivyo wanapswa kutii wajibu huo la sivyo vitafungiwa na hakuna huduma itakayokuwa inafanyika.

Taarifa imeeleza kuwa Mwakibibi amesema tayari ameshatuma timu yake kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kujua wanadai fedha kiasi gani.

Aidha, Mwakibibi ameeleza kuwa Azam wameshaonesha dalili ya kulipa na kilichobaki ni wao kutimiza sharti hilo la kulipa siku yoyote kuanzia leo.

Kiongozi huyo amekitaja kiwango cha kodi kitaanza 50,000/= mpaka 100,000/= kwa kutegemeana na ukubwa wa tukio linalokuwa linafanyika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic